Categories
changes Constructive thinking life mentality and mental health Swahili Episodes

Life, Love, Levels

Life is too short, and we have to live it to the fullest so how do we define Life itself and then how do we fight to have a balance. How do we live to the fullest?

Life to some is more of people, many people think that life is a tendency of considering happiness of others before their own, and some conclude by linking love and life.

To some life is all about them having a total brand by defining their standards so it makes them easier to them to avoid unnecessary things in the end so this group links with the levels

So after that we have establish its more of a linear relationship between life, love and levels.

Love is all about a complex topic, If you decide to explain it that’s a broad topic to cover, but for some people love is just a simple topic. But on the long run we have to  accept that love has no formulae at all.


If ego, selflessness and pride takes over any particular party in any type of relationship whether its a friends or lovers the boyfriend and girlfriend thing. Love is intertwined to levels because all these ego stuff is all principles or standards set by people and hence the portion of love intersect to levels.


Some notable quotes are as follows,
We fail to distinguish between love and pity, we are scared to have to isolate ourselves in toxic relationship but we hold on in the name of patience.

Kila mtu ana path ake no matter how similar you’re with someone else…(life against life)

We should place ground rules for friendship, lazima kuwepo na ground rules
Standards you put on having people kwa circle yako
(Life against levels)


In love, what do you really look for?
Is it peace, money,  stability,  security, friendship?


Wanawake wakiwa heartbroken wanaanza uza nguo status 😂😂😂😂




If we define what life is, love is, levels are we hope to have a best life ever, but that’s not it there are always problems.
Now question is how do you counteract your problems?

Some do panic, some take it easy knowing that problems are inevitable,  some take time to understand the bigger picture that comes with the problem

_” napata matatizo ila matatizo hayanipi matatizo … “_


Level yako unajua ww mwenyewe
Ila watu wanavyomuweka ni jinsi unavyojionyesha kwao.. ( What is your brand when your off the room, what do people say about you..?)

Love have no condition it come naturally
Upendo unaisha….

Take outs from
Nights shots
11th September


Unanswered questions
How do you identify toxic relationship?
How long should you hold on to a toxic relationship?
Why do men never let go of their ego easily ?

Categories
Swahili Episodes

Mawazo Huru

Watu wanasema mchezo kwa nje ni mrahisi , ila ingia ndani uone au ucheze.

pia kuna ka-msemo kapo kanasema ukikaa kimya utasikia mengi ukiongea utatoa tu yale uyajuayo. Kwenye usafiri wa umma mara nyingi ndipo tunasikiaga vitu vingi na mengine tunajifunza.

sasa Leo nimevutiwa na mada uliyokuwa inaendelea juu ya mifumo ya ajira na elimu, mada hyo ilikuwa inaongelewa huku mimi nikiwa nashauku kubwa ya kusikia na kujifunza na si kusema wala kuchangia.

Raha ya mada hii kila level ya watu iliwakilishwa, wazazi na wanafunzi na wahitimu wasaka ajira.

maoni yao ni kama yafuatayo.
wazazi wanasema kwamba watoto wao wanaondoka wakiwa wadogo na wanarudi nyumbani baada ya muda mrefu wakiwa wamemaliza elimu ya chuo wakiwa wakubwa ila shida wanarudi wanasubiria kuajiriwa. Akaendelea kusema ni bora kungekuwa na masomo ya ujasiriamali katika shule na vyuo vyao hukoo.

(mtazamo wangu ni sawa kuwaza ivyo na vyuo vingi wanafanya kufundisha elimu ya ujasiriamali japo wanafunzi ndo hawana mawazo ya kujiongeza ila juhudi za kujenga akili za kibunifu ni juu ya mwanafunzi. Mwanafunzi akijijenga juu ya connection hapo hatoboi ndo tunapata jamii ya kusubiri mambo yao yaende pasipo mafanikio.)

kwa upande wa wahitimu. wahitimu yapo makundi mawili waliotoka kutoka diploma na degree. sasa wengi wanalalamika ajira mtaani amna na haya yote ni kisa serikali na taasisi ziajirizo hazitoi nafasi, na endapo zitatoa zinataka watu wenye uzoefu wa miaka si chini. ya mitatu kuendelea.

(mtazamo wangu ni kwamba mimi pia nashangazwa na nafasi zitolewazo kudai uzoefu na pia nafasi huwa nyingi, ila wahitimu tunapaswa kuwa wavumilivu ni bora kujenga jina kwa kujitolea pasipo malipo, na pia wengi tunafeli kwa uwoga wa kujaribu kutafuta kazi. wengi kwa uwoga wa kutokuwa wazoefu, embu tujaribu kuomba nafasi halafu tukajitengenezee jina angalau tuweke cv zetu kwenye ofisi zao ili pindi ikitokea nafasi ingine, sura yako si ngeni.

soko la ajira sasa hivi sawa ni gumu na si rahisi kama zamani na tukae tukijua kuwa wazazi wetu au walezi hawajapitia zama za kukosa kazi kihivyo, kipindi chao walikuwa elimu ndogo na kazi zipo. kwa hyo wahitimu wajiandae kisaikolojia kwa kukabiliana na wazazi wao.)

kwa upande wa wanafunzi walioko kwenye maandalizi ya kuingia mtaani. walikuwa wako kimya kwenye mdahalo ila mtazamo wangu ni huu, chuoni ndo sehemu ya kujiconnect na wadau wako. usiache hao marafiki usipoteane hao ndio marafiki watakaokuweka mjini pale unaposaka ajira.

pia usisite kujitolea pale nafasi zinapotokea, kaa vizuri na walimu wako hao ndio watakao kuweka pia mjini , nafasi nyingi zinapitia kwao za kazi pia kuwa na namba zao.)

haya yote ni mawazo huru na ni mawazo yangu ni ruksa kupinga au kurekebisha.

Je ww uko kwa kundi gani kati ya haya tuongee kwenye kiboxi la maoni
. na pia sio kila kitu cha kuchukua katika hili chagua size yako beba fanyia kazi kama yanafaa..

Categories
Swahili Episodes

Mbele Kupo…

Kama jana nilikuacha unaelea basi nakuomba radhi ila soma tena halafu uendelee na ya leo.
Leo naanza kwa kusema ni jana tuliongelea vitu vichache kuhusu maisha baada ya chuo kuingia mtaani.
Haijalishi umechelewaje kufanya mambo ila kama imepangwa utoboe lazima utatoboa.

Tuongee uhalisia kuna watu makundi mawili pindi chuo kinafunguliwa au masomo yeyote yanapoanza.

Kundi la kwanza na la pili ni kama yafuatayo.
ni wale wanaojua wanasoma nini na wanajua nini kinawapeleka shule, halafu kuna kundi la watu wanaenda shule kwa sababu ndiyo hatua (the next stage) wanayotakiwa kuchukua. Mimi kiukweli sijui ulikuwa stage gani ila hapa ndio hatua ya kwanza ya kuweza kujisaidia kuingia mtaani.

Sasa kama ulikuwa unajua unafanya nini shule au huelewi mimi sio jaji wa maisha ila kuna jambo la kuchunguza mara nyingi kwa sisi ambao hatujielewi ni presha tulionao kutoka kwa mazingira tuliotoka ikiwemo kama mzazi mlezi au ndugu haya yote yanaletwa kwa sababu zifuatazo ninazozielewa

Kwanza Mifumo yao wanataka iwe yetu:
Kila mtoto au kila mtu ana mfumo wake wa malezi ukiangalia familia zenye mtoto zaidi ya mmoja ukiangalia wazazi ni wale wale ila kila mtoto ana namna ya malezi. sasa hili watu wengi hawajui na tunaishia kuona kama kila jinsi mtu anavyoishi ndivyo na sisi tunabidi tuishi. Hapana. “haijalishi umechelewaje kufanya mambo ila kama imepangwa utoboe lazima utatoboa” usijifananishe namna yako ya maisha
na namna ya maisha ya mtu mwingine. Si laumu ila wazazi wengi wanataka watoto waunge tela. wawe pale nyuma yao wafanye vile vile walivyofanya wakiwa vijana. Kama alikuwa daktari atataka mtoto wake awe daktari kwa hyo inabidi mtoto afuate kila njia aliyopitia.

Ya Majirani Kwetu
Saa ingine mafanikio au maneno ya watu huleta adhari kwenye maamuzi ya walezi au hata wazazi wetu. Utasikia wewe fulani kuwa kama mtoto wa fulani unaona kaenda chuo kachukua engineering kawa mtu wa serikali, bila kujali hata mtoto anataka nini sasa haya huleta shida kwa mtoto bila hata mzazi kujua kwa haraka.

Madhara yake ni wazi kwa maisha ya watoto mfano ni ngumu kufanya maamuzi binafsi.
Embu mtafute mwanafunzi aliyemaliza chuo kwa ngazi ya diploma au degree kwa haraka haraka muulize nini kinafuata? wengi watakuambia hawajui na wengi wanaona njia rahisi ni kuendelea kusoma si semi kusoma si jambo zuri ila naona kama ni njia ya kukimbia ukweli. jana tuliona suala zima la deadlines as mtu yuko rahisi kuendelea
kusoma kisa ndo njia rahisi kwake kuwa na control ya mambo yake. Ukiwa shule unnaweza kuwa na usukani wa mambo kisa ni mambo machache tu unayofanya ambayo utawaza tu ada,modules na wapi utapata chakula, mavazi na wapi utalala. ila mtaani life haieleweki mambo yanakuwaga mengi kiasi wengi wanaogopa ingia mtaani kupambana

Categories
Swahili Episodes

Naenda, Ila Panaboa

Je life la kitaa vipi?
Wakati wote tumeshazoea kuwa na mipango endelevu
Tunapenda kuwa na uwezo wa kuhimili shida zijazo mbele zetu.
lakini mara nyingi hatuna uwezo kwa asilimia zote kuzuia kwa asilimia 100
mara nyingi zinakuwa sio shida zetu ila ni mipango ambayo haijakaa fresh.

Mazoea yetu kila siku yanajenga tabia ambayo mara kwa mara inakuwa ngumu kukwepa au sahau mapema. Kwanza ni jambo la kushukuru Mungu kwa hapo ulipofika, uzima afya na nguvu ulionayo sio mipango yako ila kila kitu kinaenda poa. Tuna uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa kwa kuthibiti vyakula tulavyo na hata kufanya mazoezi.

Nilipishana na mwanachuo aliyekuwa amepaki vitu vyake ili aende nyumbani,
nikamuuliza vipi mbona unaonekana hauna raha wala kama vile hutaki kwenda huko unapokwenda. ndiye aliyenijibu
ninaenda ila panaboa.

Baada ya kumaliza mitihani yangu nimekuwa na mud amrefu kusikiliza watu walionitangulia, walioko na hali kama mimi na hata kusikiliza watu na mawazo tofauti tofauti. kila mtu ana usemi wake juu ya mambo tofauti tofauti ni sisi kusikiliza nna kujifunza

Mwanzo nilicheka ila baada ya muda mawazo yakanijia ya kwanini anasema kuwa nyumbani kunaboa?
Naomba niongee na wewe uliyemaliza chuo kwa ngazi yeyote na hauna mwelekeo haswa upi unaweza kutumia ili utoboe kwanza mimi sipo hapa kukupa mchongo ila nakuambia nilichojifunza kati ya wiki moja au mbili.

Deadline:

Katika maisha ya kiwanafunzi tumezoea kuishi kwa deadline, naweza sema deadline ni hali au ka kamba kadogo ambacho tunajitahidi kufanikisha mambo huku tunaning’inia kwa hiyo kamba. mara nyingi ubora wa kazi hauwi mzuri kisa ya kufanya kazi kwa pressure. Muda hatuutumii ipasavyo na hili tumelichukulia sawa
tu kisa ni mazoea, mazoea ni vyema kuyajenga ila tuaangalie tunajenga nini na tunajengea wapi. Sasahivi inakuwa ngumu kuanza maisha mtaani kisa mtaani hamna deadline kama shule na pia hakuna mtu wa kusimamia au kuweka uzito ule kama wa shule, na hii hali unakuta mtu yuko radhi kutamani kurudi shule baadala ya kuhustle mtaani.

Kupokea Pokea:

Chuoni kama ulikuwa unapokea mkopo hapa naomba niongee na wewe sio mbaya ila mazoea yaambatanayo na maisha unayoishi ya mkopo ndo tunayangalia.
mkopo unatumia sawa na boom ulikuwa nalo so umejizoesha kwamba hela ipo. na wengi tumezizoeza kwamba hela ipo na mara nyingi ni rahisi kumiss chuo kisa ya hela kuingia kirahisi rahisi.Mtaani usiingie na mtazamo huo utakata maini mapema na kuona mtaa mchungu.

Connections:

Umemaliza shule na unategemea connection ndo zitakuweka mjini, sawa kama hizo connection umejijengea mwenyewe hapo sawa ila kama ni connections ambazo ni
ndugu au wazazi au watu wa karibu wamezitengeneza na wewe unategemea kuishi nazo embu acha kuweka matarajio makubwa hapo. ukiwa chuo hicho kizazi ulichonacho au watu wanaokuzunguka ndio hao watakutoa katika hali uliopo ndo muda haswa wakutengeneza michongo na dili za kuelekweka . na usije sema nyumbani utapata michongo. Nyumbani hakuna michingo ukikaa nyumbani utajipotezea uukaribu na hawa watu. Na mara nyingi tunakuwa na level tofauti katika maisha kisa ya kujitenga na wanafunzi wenzetu, walimu na hata watu wengine .

ITAENDELEA

Design a site like this with WordPress.com
Get started