Categories
Swahili Episodes

Mawazo Huru

wengi wetu hatuna shida ni kwamba tuna kelele nyingi juu ya shida ndogo

Watu wanasema mchezo kwa nje ni mrahisi , ila ingia ndani uone au ucheze.

pia kuna ka-msemo kapo kanasema ukikaa kimya utasikia mengi ukiongea utatoa tu yale uyajuayo. Kwenye usafiri wa umma mara nyingi ndipo tunasikiaga vitu vingi na mengine tunajifunza.

sasa Leo nimevutiwa na mada uliyokuwa inaendelea juu ya mifumo ya ajira na elimu, mada hyo ilikuwa inaongelewa huku mimi nikiwa nashauku kubwa ya kusikia na kujifunza na si kusema wala kuchangia.

Raha ya mada hii kila level ya watu iliwakilishwa, wazazi na wanafunzi na wahitimu wasaka ajira.

maoni yao ni kama yafuatayo.
wazazi wanasema kwamba watoto wao wanaondoka wakiwa wadogo na wanarudi nyumbani baada ya muda mrefu wakiwa wamemaliza elimu ya chuo wakiwa wakubwa ila shida wanarudi wanasubiria kuajiriwa. Akaendelea kusema ni bora kungekuwa na masomo ya ujasiriamali katika shule na vyuo vyao hukoo.

(mtazamo wangu ni sawa kuwaza ivyo na vyuo vingi wanafanya kufundisha elimu ya ujasiriamali japo wanafunzi ndo hawana mawazo ya kujiongeza ila juhudi za kujenga akili za kibunifu ni juu ya mwanafunzi. Mwanafunzi akijijenga juu ya connection hapo hatoboi ndo tunapata jamii ya kusubiri mambo yao yaende pasipo mafanikio.)

kwa upande wa wahitimu. wahitimu yapo makundi mawili waliotoka kutoka diploma na degree. sasa wengi wanalalamika ajira mtaani amna na haya yote ni kisa serikali na taasisi ziajirizo hazitoi nafasi, na endapo zitatoa zinataka watu wenye uzoefu wa miaka si chini. ya mitatu kuendelea.

(mtazamo wangu ni kwamba mimi pia nashangazwa na nafasi zitolewazo kudai uzoefu na pia nafasi huwa nyingi, ila wahitimu tunapaswa kuwa wavumilivu ni bora kujenga jina kwa kujitolea pasipo malipo, na pia wengi tunafeli kwa uwoga wa kujaribu kutafuta kazi. wengi kwa uwoga wa kutokuwa wazoefu, embu tujaribu kuomba nafasi halafu tukajitengenezee jina angalau tuweke cv zetu kwenye ofisi zao ili pindi ikitokea nafasi ingine, sura yako si ngeni.

soko la ajira sasa hivi sawa ni gumu na si rahisi kama zamani na tukae tukijua kuwa wazazi wetu au walezi hawajapitia zama za kukosa kazi kihivyo, kipindi chao walikuwa elimu ndogo na kazi zipo. kwa hyo wahitimu wajiandae kisaikolojia kwa kukabiliana na wazazi wao.)

kwa upande wa wanafunzi walioko kwenye maandalizi ya kuingia mtaani. walikuwa wako kimya kwenye mdahalo ila mtazamo wangu ni huu, chuoni ndo sehemu ya kujiconnect na wadau wako. usiache hao marafiki usipoteane hao ndio marafiki watakaokuweka mjini pale unaposaka ajira.

pia usisite kujitolea pale nafasi zinapotokea, kaa vizuri na walimu wako hao ndio watakao kuweka pia mjini , nafasi nyingi zinapitia kwao za kazi pia kuwa na namba zao.)

haya yote ni mawazo huru na ni mawazo yangu ni ruksa kupinga au kurekebisha.

Je ww uko kwa kundi gani kati ya haya tuongee kwenye kiboxi la maoni
. na pia sio kila kitu cha kuchukua katika hili chagua size yako beba fanyia kazi kama yanafaa..

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started